• Salamu María, umejaa neema,

    Bwana yu nawe.

    Umebarikiwa kuliko wanawake wote,

    na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.

    Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu,

    utuombee sisi wakosefu,

    sasa na saa ya kufa kwetu.

    Amina.

  • Sala Ya Kujiweka Wakfu Kwa Moyo Safi Wa Maria

    Mimi… (Jina) mkosefu, maskini mwenye imani haba, siku ya leo ninafanya tena upya ahadi zangu za Ubatizo, nikijiaminisha katika mikono yako, Pa Moyo Safi wa Bikira Maria. Ninamkataa shetani daima na mambo yake yote na kazi zake na ninajitolea kabisa kwa Yesu Kristo, hekima ya umwilisho, kwa kuubeba msalaba wangu na kumfuata siku zote za maisha yangu. Na nitakuw mwaminifu kwake zaidi tangu sasa, kuliko nilivyofanya zamani.

    Mbele ya Jeshi lote la mbinguni, leo nimekuchagua wewe uwe Mama na msaada wangu. Nitajitoa na kujiweka wakfu kabisa kwako, kama mtumwa wako, mwili na roho yangu, mema yangu, ya ndani na nje, na hata yale matend mema, ya zamani, ya sasa na wakati ujao; nikikuachia kila kitu hata haki zangu zote na yote yaliyo yangu bila kubagua; uyatumie yote upendavyo, kwa ajili ya utukufu zaidi wa Mungu, kwa sasa na milele. Amina.

  • Sala Kwa Moyo Mtakatifu Wa Yesu

    Ee Moyo Mtakatifu sana wa Yesu, chemchemi ya kila baraka, ninakuabudu wewe na pamoja na sikitiko la kweli kwa ajili ya dhambi zangu, ninakutolea moyo wangu huu maskini. Nifanye niwe mnyenyekevu, mvumilivu, msafi na mtiifu kabisa kwa mapenzi yako. Yesu mwema nijalie niishi katika wewe kwa ajili yako. Unilinde katika hatari zote, unifariji katika huzuni zangu, unipatie afya ya mwili, msaada katika mahitaji yangu, baraka zako kwa yote nitakayofanya, na neema ya kifo kitakatifu. Amina.